RSS Feed

Tag Archives: Serengeti

MALIASILI ZETU: Tunaweza kupiga hatua, tukiamua

Posted on

Ngorongoro, Serengeti, Selous, Mkomazi, Mikumi, Manyara, Kituro, Udzungwa, Katavi, Gombe, Mahale, Lukwika-Lumesule, Arusha (ANAPA), Kilimanjaro (KINAPA), Tarangire, Saadani. Bulyankulu, Mwadui, Nyamongo, Buzwagi, Barrick, Geita, Uvinza, Kiwira, Mchuchuma na Songosongo.

Nilikuwa nawaza hivi: Tanzania ina maliasili na rasilimali nyingi sana. Na rasilimali zetu hizi zote ni pesa tupu. Na tukiamua na kuwa na dhamira ya kweli tunaweza kuzitumia maliasili zetu hizi hizi kuwakwamua Watanzania katika lindi la umaskini.

Nilikuwa nawaza hivi: Tunaweza kujiwekea lengo kwamba mapato yetu ya mwaka mzima kutoka Serengeti na Ngorongoro tutayatumia kujenga barabara ya lami kutoka Mugumu kwenda Tarime kupitia Nyamongo. Halafu tunaweka vibao vikuuuuubwa: “Barabara hii imejengwa kwa mapato na faida iliyopatikana katika hifadhi za Serengeti na Ngorongoro.

Halafu mapato ya mwaka mzima ya mbuga za Saadani, Ruaha, Katavi na Udzungwa, badala ya kupelekwa hazina; tukatumia hiyo pesa yote kujenga kipande cha barabara kuunganisha mkoa wa Rukwa na Mbeya au kuunganisha mkoa wa Iringa na Dodoma. Halafu tunabandika sign kuuubwa inayosema: “Barabara hii ya lami imejengwa kwa mapato yatokanayo uhifadhi wa wanyapori katika hifadhi za Taifa za Saadani, Ruaha, Katavi na Udzungwa.

Hivyo hivyo tukatumia mapato ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu na Nyamongo kujenga barabara ya lami kutokea kutokea Muleba kupitia Biharamulo, Geita, Sengerema mpaka Mwanza. Yes. Halafu tunaweka booonge la advertise: “The North-West Madini Boulevard.” Atakayetaka kuendesha pikipiki yake kutoka Bukoba hadi Mwanza, haya. Atakayetaka kuendesha ki-Toyota Corolla chake kutoka Iringa hadi Rukwa, haya. Mkulima wa Nkasi akitaka kununua Fuso yake na kusafirisha mahindi yake kwenda Mbeya, haya.

Tukiamua, tunaweza kuwa na miradi ya maendeleo tunayoifadhili kwa pesa yetu wenyewe. Mungu ibariki Tanzania.

I love Tanzania

Posted on

ASANTE SANA MSOMAJI WANGU WA SERONERA (SERENGETI) KWA KUNITUMIA HII:

By Chunde, Serengeti 2006

Fahari yetu

Down the memory lane

Posted on
In Serengeti in 2005: L to R: Chunde, Anne, Mrs Chunde, Michael and Kiongozi

In Serengeti in 2005: L to R: Chunde, Anne, Mrs Chunde, Michael and Kiongozi

Ah. Siku zinakimbia sana. Hii ilikuwa mwaka 2005 wakati kiongozi anaishi Seronera, Serengeti.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.