Kama yaliyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 31 Machi 2011 ni (madai) ya kweli, basi serikali imeamua kuligeuza mtaji suala zima la uundaji wa katiba mpya. Na kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kina idadi kubwa ya wabunge ambao hawawezi kuthubutu kuukataa mswada ulioletwa na serikali ya chama chao, basi kelele zote za katiba mpya zitatupwa kwenye kapu la historia kama “uthubutu”! Inasikitisha.
Tag Archives: Rais wa Tanzania
Ah?

Msimu wa tu-ku-tu-ku-tu-ku-tu-ku
Jana Mh. Rais ameagiza mitambo ya IPTL iwashwe ili kutunusuru na janga la giza totoro. Niliposikia hilo agizo lake nilishtuka kidogo. Kilichonishtua: 1) Ina maana ile mitambo ipo tu imezimwa wakati sisi tunalala gizani? 2) Mbona waziri wake juzi alidai kwamba amekuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa IPTL ili turuhusiwe kuibadilisha mitambo yao kutoka kutumia mafuta hadi kutumia gesi?
Mi nimechanganyikiwa.


