RSS Feed

Tag Archives: pesa

Mambo mengine si kwa sababu ya umaskini

Posted on

Watanzania wengi tumekuwa tukitafuta ulaji badala ya kutafuta kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi yetu. Utamkuta mtu anakuuliza: “Siku hizi uko wapi?” Unamwambia: “Ninafanya kazi BOT.” Au: “Nipo mamlaka ya mapato Tanzania.” Au wakati mwingine unamweleza: “Ninafanya kazi na ubalozi wa Finland.” Atakachokujibu sasa utashangaa. Mara zote nimekuwa nikisikia watu wakiniambia: “Aisee, huko ndo kwenye pesa. Mambo yako safi sana mzee.” Ukijaribu kuwahoji wanachomaanisha si pesa halali ya mshahara. Bali ni zile pesa waweza kuzipata kama wewe ni mtu wa dili.

Mawazo haya ya dili yatatufikisha wapi?

Saa ya mabadiliko ni sasa

Wakati umefika wa kuwa na katiba inayo-cover changamoto tunazokumbana nazo leo

Wakati umefika wa kuwa na katiba inayo-cover changamoto tunazokumbana nazo leo

Matatizo na changamoto kadhaa tunazokutana nazo leo zinahitaji kuwa na sheria-mama inayoweza kupambana nazo. Kuna mambo mengi yanaendelea kujitokeza hapa Tanzania, hasa ya kimaadili ya uongozi na utawala bora, ambayo katiba yetu ya sasa ama haisemi au inasema kwa namna ambayo haiwezi kutufanya kuwa na viongozi wenye kuzingatia maadili na misingi ya utawala bora.

Tuchukulie mfano mmoja ambao mimi binafsi unanichefua sana. Watu wanatuhumiwa kwa ufujaji/wizi wa mali/pesa za nchi lakini bado unaona wamekaa bungeni.

Jamaa hao hao wanaohusishwa na wizi wa mali za nchi bado wamekaa kwenye chombo cha kutunga sheria. Hii ni hatari. Mtu leo anang’atuka/anajiuzulu kwa kashfa mbaya ya wizi wa mali za Watanzania lakini unamwona bado anachangia mijadala bungeni.

Meseji tunayotuma kwa wapiga kura wake ni hii: huyu bwana yuko safi ila sema tu tumempiga stop. Vichekesho.

Tunatakiwa kuwa na sheria inayosema hivi: kiongozi wa serikali wa ngazi yoyote anapokuwa amehusishwa kwa namna yoyote na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora atasimamishwa mara moja kufanya kazi za kiuongozi katika nchi hadi hapo vyombo husika vitakapom-declare kwamba yeye ni safi.

Naomba kuto hoja.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.