RSS Feed

Tag Archives: Mwanza

MALIASILI ZETU: Tunaweza kupiga hatua, tukiamua

Posted on

Ngorongoro, Serengeti, Selous, Mkomazi, Mikumi, Manyara, Kituro, Udzungwa, Katavi, Gombe, Mahale, Lukwika-Lumesule, Arusha (ANAPA), Kilimanjaro (KINAPA), Tarangire, Saadani. Bulyankulu, Mwadui, Nyamongo, Buzwagi, Barrick, Geita, Uvinza, Kiwira, Mchuchuma na Songosongo.

Nilikuwa nawaza hivi: Tanzania ina maliasili na rasilimali nyingi sana. Na rasilimali zetu hizi zote ni pesa tupu. Na tukiamua na kuwa na dhamira ya kweli tunaweza kuzitumia maliasili zetu hizi hizi kuwakwamua Watanzania katika lindi la umaskini.

Nilikuwa nawaza hivi: Tunaweza kujiwekea lengo kwamba mapato yetu ya mwaka mzima kutoka Serengeti na Ngorongoro tutayatumia kujenga barabara ya lami kutoka Mugumu kwenda Tarime kupitia Nyamongo. Halafu tunaweka vibao vikuuuuubwa: “Barabara hii imejengwa kwa mapato na faida iliyopatikana katika hifadhi za Serengeti na Ngorongoro.

Halafu mapato ya mwaka mzima ya mbuga za Saadani, Ruaha, Katavi na Udzungwa, badala ya kupelekwa hazina; tukatumia hiyo pesa yote kujenga kipande cha barabara kuunganisha mkoa wa Rukwa na Mbeya au kuunganisha mkoa wa Iringa na Dodoma. Halafu tunabandika sign kuuubwa inayosema: “Barabara hii ya lami imejengwa kwa mapato yatokanayo uhifadhi wa wanyapori katika hifadhi za Taifa za Saadani, Ruaha, Katavi na Udzungwa.

Hivyo hivyo tukatumia mapato ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu na Nyamongo kujenga barabara ya lami kutokea kutokea Muleba kupitia Biharamulo, Geita, Sengerema mpaka Mwanza. Yes. Halafu tunaweka booonge la advertise: “The North-West Madini Boulevard.” Atakayetaka kuendesha pikipiki yake kutoka Bukoba hadi Mwanza, haya. Atakayetaka kuendesha ki-Toyota Corolla chake kutoka Iringa hadi Rukwa, haya. Mkulima wa Nkasi akitaka kununua Fuso yake na kusafirisha mahindi yake kwenda Mbeya, haya.

Tukiamua, tunaweza kuwa na miradi ya maendeleo tunayoifadhili kwa pesa yetu wenyewe. Mungu ibariki Tanzania.

Mwanza!

Posted on

(c) Mwemezi 2008

The Rock City — Mwanza

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.