Kwa miezi kadhaa tumekuwa au tukisikia, kuona au kusoma juu ya milipuko ya mabomu katika eneo la Mbagala jijini Dar es salaam. Wengi wetu hatuendi mbali zaidi kuona nyuma au ndani ya milipuko hii kuna nini. Kinachotokea Mbagala leo kinaweza kutokea Lugalo, Monduli au Ruvu siku za usoni.
Miji na makazi yetu hapa Tanzania yanaongoza kwa kukaa shaghalabaghala (not planned). Mamlaka zinazohusika na mipango miji/vijiji ni kama vile hazipo. Tunaishi katika ardhi ambayo haijawahi kupimwa na wala hii ardhi si yetu. Sheria ya ardhi ya Tanzania haimtambui Mtanzania kama mmiliki wa ardhi; hata kama amejenga hapo anapoishi na kupaita kwake. Ardhi ni mali ya serikali – jamhuri.
Hii imepelekea watu kwenda na kujipatia ardhi katika maeneo ambayo zamani yaliwahi kuwa makambi ya jeshi. Hiki ndo kinachotokea Mbagala. The area (now residential) used to be a barracks! Kwa kadri watu wanavyoendelea kufanya shughuli zao ndivyo wanavyoendelea kuyachemsha mabomu ambayo ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi (improper disposal) yaliachwa siku za nyuma.
Kwa sababu tunaishi katika maeneo ambayo hayajawahi kupangwa au kupimwa, matukio kama haya hatuwezi kuyaepuka.


