
Sustainable energy is still a huge problem across Tanzania
Nakumbuka mtangazaji mmoja maarufu wa VOA aliwahi kuja Afrika kufanya interviews na marais wetu. Mojawapo ya maswali aliyokuwa akiuliza lilikuwa hivi: “Mheshimiwa Rais, umekuwa kiongozi wa nchi hii kwa kipindi kirefu sasa; ni jambo gani moja tu ambalo unadhani wananchi wako watakukumbuka kwalo?
Kitu ambacho kilimshangaza sana yule mtangazaji ni kwamba karibu marais wote wa Afrika aliowahoji (wakiwemo wastaafu), hakuna aliyeweza kujibu swali hilo kiufasaha.
Marais wetu hawajui jambo moja (moja tu) ambalo wananchi wao watalikumbuka watakapokuwa wametoka madarakani. Hata wakishastaafu hawajui ni kitu kitu gani kimoja waliwafanyia wananchi na bado kinakumbukwa.
Kila aliyemwuliza alianza “Oh unajua nimefanya mambo mengi, siwezi kuyataja yote.” Na blah blah kibao.
Lakini tuseme tu ukweli. Marais wetu wanaingiaga madarakani bila malengo. Hakuna jambo moja ambalo anakuwa nalo kwamba angetaka kulifanya. Na madhara yake wanagusa kila kitu na mwisho wa siku wanakuwa hawajafanya lolote la maana.
Au wakiamua kufanya kitu, wanaibuka na madudu ambayo huwezi kupima mafanikio yake, kwa mfano MKUKUTA, MKURABITA, KASI MPYA, KILIMO KWANZA. Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuketi chini baadae na kupima kama vimefanikiwa au la – they are vague goals.
Ni tofauti na Rais ambaye anasema (tena kutoka moyoni) kwamba: “Mimi wakinichagua tu, nitahakikisha tunatandaza barabara za lami hadi kila makao makuu ya wilaya. Ndani ya miaka yangu kumi ya uongozi hata kama nitashindwa kila kitu ila nitahakikisha wilaya zote za Tanzania zinafikika kwa lami.” Sasa, huyo ni kiongozi.
Au mwingine anaweza akasema, “Mimi wakinichagua nitahakikisha kukosa nishati endelevu (umeme, gesi, solar, nk) hapa nchini kwetu inakuwa ni historia. Nitahakikisha tunapata umeme kwa gharama nafuu na nishati nyinginezo endelevu zinakuwa affordable.”
Wito na ombi langu ni kwamba ifike wakati sisi tunaokimbilia kugombea nyadhifa mbalimbali tujiulize: hivi ni nini nitalifanyia taifa langu endapo nitachaguliwa? Nitafanya jambo gani moja ambalo nitakumbukwa kwalo?
Ni jambo moja tu. Sio mambo lukuki.

