RSS Feed

Tag Archives: Kiingereza

wao waweze wana nini? Na sisi tushindwe tuna nini?

Posted on

Leo kanisani kwetu alikuja mgeni. Ni baba Mmarekani ambaye, kwa mujibu wake mwenyewe, ameishi Tanzania kwa miaka takriban 14. Alipewa nafasi ya kuhubiri — mada kuhusu watoto. Mimi kama ilivyo kawaida yangu nikadhani kungekuwa na mtafsiri wa mahubiri yake.

Huyu baba alinishangaza. Alipoanza kuongea tu: lafudhi, vibwagizo, misemo, majigambo, nahau — utadhani ni Mswahili wa Bagamoyo. Kiswahili safi kabisa. Kwa mtu ambaye angekuwa akisikiliza akiwa nje bila kuona rangi ya ngozi ya huyu baba asingeweza kuamini kwamba anayehubiri kanisani ni Mmarekani.

Huyu amejifunza lugha yetu ndani ya miaka ipatayo kumi na nne tu na ameiwezea kabisa. Hachanganyi neno la Kiingereza hata moja. Anaongea kama sisi: mimi na wewe. Bila shida yoyote.

Baadae nikaanza kutafakari na kujiuliza. Sisi tunaanzaga kujifunza lugha ya wenzetu (Kiingereza) tukiwa darasa la tatu. Kwa hiyo tunapomaliza darasa la saba huwa tumejifunza Kiingereza kwa miaka takriban minne. Halafu tunaanza masomo ya sekondari: tunajifunza Kiingereza kwa miaka minne hadi sita. Jumla? Miaka kumi. Kisha tena kuna wanaobahatika kuendelea na masomo ya Chuo kikuu kwa miaka mitatu hadi mitano (5). Jumla? Miaka kumi na mitano!!! Lakini kisikie hicho Kiingereza chetu. Duh! Penye “the” tunasema “ze”. Sentensi zetu zina “is” kibao.

Lazima tukiri tu. Sisi ni wavivu wa kujifunza. Tunafanya ili mradi tu. Hatutafuti kufanya mambo sawa sawa. Tunatafuta njia za mkato na kufaulu mitihani. Hayo ni mawazo yangu tu.

Kama wao wanaweza kujifunza na kuimudu lugha yetu. Sisi pia TWAWEZA.

Kama Kiswahili ni lugha ya Taifa mbona masuala mazito ya Kitaifa yanaandikwa kwa Kiingereza?

Posted on

If, and this is constitutional, Kiswahili is our National language, why do we write matters of national concern in English? Weird!

 

Kiinglish: Kwani lazima?

Posted on
Filamu Zetu

Filamu Zetu

Hiki nacho ni kichefuchefu kingine. Sasa hivi wasanii wetu hasa wale waigizaji wa filamu pamoja na maprodyusa wao wameibuka na jipya. Filamu karibu zote wanazoigiza sasa hivi zinatoka kwa majina ya Kiingereza. Mwanzoni nilifikiri labda jamaa wanaongea kiinglish humo ndani. Kucheki nikakuta wanapiga Kiswahili muvi nzima. Sasa kwa nini wanaipa jina la kidhungu wakati kinachoongewa humo ni Kiswahili?

Majina ya filamu zinazotoka sasa hivi ni kama: Last Minutes, My Love, Don’t Hurt Me, n.k

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.