Rafiki yangu kwenye facebook alinitumia meseji hii (by accident):
Pia kumbuka kaka kuwa anayofanya Lipumba ni dalili ya aliyechoka na yuko sokoni kunadi bidhaa mbovu inayotia ukakasi masikio ya wateja.
Cuf kwa kuwananga CHADEMA wakati walishajigamba kuwa wao ni wapinzani inajionyesha wazi kuwa sasa CUF ni CCM B na hakuna shaka juu ya hilo.
Wapenzi wa CUF wakae na kutambua kuwa wao ni sehemu ya CCM kwa kutekeleza sera na mikakati. Maalimu kule Zanzibar anatekeleza ilani ya CCM na Lipumba huku bara anashambulia chama kikuu cha upinzani kama inavyofanya CCM.
Lipumba anasumbuliwa na mchoko wa kisiasa ambao umesha ongeza kasi ya kukidhoofisha chama hicho kwa huku bara. CUF iliyowahi kujitambulisha kama chama ngangari leo hii kimegeuka chama mdebwedo na mlenda kwa kukubali kutumiwa na CCM na wao kujikuta wameingia mtegoni na sasa wao kama wanandoa wanahami unyumba wao usitetereke.
CHADEMA ndio ninao amini kuwa ni wapinzani wa kweli na watetezi waliobeba matumaini ya watanzania.