RSS Feed

Tag Archives: CHADEMA

Hiyo Nakala ya Mswada wa Katiba Mpya inapatika(je) wapi?

Posted on

Jana kulikuwa na Kongamano la Katiba kwenye Ukumbi wa Nkrumah, UDSM. Na, nilivyosoma katika magazeti ya leo, isipokuwa yale ya Chama na Serikali, ni kwamba wadau wengi walionyeshwa kukerwa na mswada utakaopelekwa bungeni mwezi huu ili mchakato wa kuunda katiba mpya uanze. Habari zilizopo zinaonyesha kwamba mswada huo una mapungufu mengi ambayo yanahitaji kurekebishwa kabla ya mswada wenyewe kujadiliwa na hatimaye kuwa sheria.

Na kwa sababu chama-tawala kina idadi kubwa ya wabunge endapo huo mswada utapelekwa hivyo hivyo: Mheshimiwa Cheyo (UDP), Lyatonga Augustine Mrema (TLP), Kafulira (NCCR), wabunge wote wa CUF na wale wa CCM wataupitisha hivyo hivyo na hatimaye itakuwa sheria. Baada ya muda mfupi tutakuja kugundua kwamba tulichotengeneza haikuwa katiba mpya bali tuliiwekea viraka ile ile ya zamani.

Wananchi tungependa kupata nakala ya huo mswada ili nasi tuisome tusipelekwe hivi hivi kiubabe. Nchi ya Tanzania ni yetu sote na si ya watu wachache ambao wako kwenye ngazi za utawala.

Habari ya jana 1: Profesa Safari ajiunga na CHADEMA

Posted on

Nilipozisikia habari za mtu ninayempenda na kumheshimu kama mwanataaluma na mwanafalsafa mzuri kati ya wanazuoni wa Tanzania, Prof. Safari kwamba amejiunga na kambi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea Chama cha Wananchi (CUF) sikushangaa sana.

Kwanza, CUF kwa siku za karibuni wamekosa ile kasi yao na ‘upinzani’ wa kweli. Matamshi ambayo amekuwa akiyatoa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibarahim Lipumba, yamekuwa yakionyesha dhahiri kwamba CUF ile tuliyoijua imebadilika na sasa imekuwa kama ‘CCM (b)’. Siwezi kuwalaumu sana CUF kwa mabadiliko hayo, nafikiri walikosea pale ambapo walishindwa kubashiri madhara ya muafaka kati yao na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Zanzibar. Wakajikuta kwenye mtego ambao na kuingia na sasa wanalipa gharama. Kwa hiyo kwa mtu yeyote ndani ya CUF ambaye angependa kushindana na siasa za CCM hana jinsi bali kutafuta uwanja mwingine.

Pili, na hii ni kama ushauri kwa uongozi wa CHADEMA. Inawezekana (mimi sina uhakika) aliye-injinia ‘muafaka’ kati ya CCM na CUF ni huyo huyo mliyepokea jana. Kwa hiyo muwe macho nyie CHADEMA isije ikawa ujio wa Safari umeandaliwa makusudi ili kupunguza makali yenu. Msiwe na haraka ya kumpa uongozi hadi hapo mtakapohakikisha kwamba huyo mtu hana ajenda ya siri. Ni tahadhari tu wala sina ‘bifu’ yoyote na profesa.

Neno kutoka kwa rafiki: CUF na CCM ni ndoa. Ndoa bila unyumba yafa

Posted on

Rafiki yangu kwenye facebook alinitumia  meseji hii (by accident):

Pia kumbuka kaka kuwa anayofanya Lipumba ni dalili ya aliyechoka na yuko sokoni kunadi bidhaa mbovu inayotia ukakasi masikio ya wateja.
Cuf kwa kuwananga CHADEMA wakati walishajigamba kuwa wao ni wapinzani inajionyesha wazi kuwa sasa CUF ni CCM B na hakuna shaka juu ya hilo.

Wapenzi wa CUF wakae na kutambua kuwa wao ni sehemu ya CCM kwa kutekeleza sera na mikakati. Maalimu kule Zanzibar anatekeleza ilani ya CCM na Lipumba huku bara anashambulia chama kikuu cha upinzani kama inavyofanya CCM.

Lipumba anasumbuliwa na mchoko wa kisiasa ambao umesha ongeza kasi ya kukidhoofisha chama hicho kwa huku bara. CUF iliyowahi kujitambulisha kama chama ngangari leo hii kimegeuka chama mdebwedo na mlenda kwa kukubali kutumiwa na CCM na wao kujikuta wameingia mtegoni na sasa wao kama wanandoa wanahami unyumba wao usitetereke.

CHADEMA ndio ninao amini kuwa ni wapinzani wa kweli na watetezi waliobeba matumaini ya watanzania.

Mchakato wa Uundaji wa Katiba Mpya waanza kutia Shaka

Posted on

Kama yaliyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la tarehe 31 Machi 2011 ni (madai) ya kweli, basi serikali imeamua kuligeuza mtaji suala zima la uundaji wa katiba mpya. Na kwa kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kina idadi kubwa ya wabunge ambao hawawezi kuthubutu kuukataa mswada ulioletwa na serikali ya chama chao, basi kelele zote za katiba mpya zitatupwa kwenye kapu la historia kama “uthubutu”! Inasikitisha.

Vita dhidi ya CHADEMA ina faida gani kwa CUF?

Posted on

CUF tuambieni ajenda yenu

Majuzi gazeti la kila siku hapa nchini lilimnukuu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akisema kwamba wanaodhani kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinaweza kushika dola na kuongoza nchi ya Tanzania labda waende kwa “Babu wa Loliondo” wakapate kikombe cha dawa.

Nilipoisoma ile habari kwanza nilishtuka. Sikujua vita ya CUF dhidi ya CHADEMA ni kubwa kiasi hicho. Pia sikutarajia mtu ninayemheshimu sana kama Profesa Lipumba; mtu ambaye kwenye chaguzi zilizopita niliwahi hata kutaka kumpigia kura anaweza kuwa na lugha za kejeli kiasi hicho. Pia sikujua Lipumba amepata wapi ujasiri wa kuongea mambo mazito kama hayo. Kwa jinsi sentensi ilivyokaa ni kama profesa ana uhakika kabisa kwamba CHADEMA haiwezi kuongoza dola. Huo uhakika ameutoa wapi?

Swali nililojiuliza mwishowe lilikuwa: CUF inapata faida gani inapoipiga vita CHADEMA?

IPP Media: Vyuo vikuu CHADEMA waja na ‘Washa Taa Mchana’

Posted on

Shauri yenu mtafunguliwa mashtaka kwamba mnataka kupindua nchi na kusabisha vita

Kama ningekuwa Kiongozi wa “Chama”/Serikali

Posted on

Hivi karibuni nchi yetu imeshuhudia sarakasi za kisiasa zinazozihusisha pande mbili. Upande mmoja ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) au serikali na kwa upande mwingine ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa yule (yeyote) ambaye amekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania tangu ulipoingia mfumo wa siasa za vyama vingi hapa nchini atakubaliana na mimi kwamba kwa sasa mazingira ya kisiasa ya nchi yetu yamebadilika sana. Mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 tulishuhudia chaguzi ambazo zilivihusisha vyama vingi. Ukilinganisha na chaguzi zote za nyuma, ule wa 2010 umekuwa ni uchaguzi ulioibua mambo mengi.

Kuna watu ambao hawakuridhishwa kabisa na namna ambavyo Tume ya Uchaguzi ya Tanzania ilisimamia uchaguzi huo. Kuna ambao wanasema hadi leo kwamba asilimia ya wananchi iliyojitokeza na hatimaye kumchagua Rais ilikuwa ndogo kiasi ambacho kinatia doa (mashaka) ushindi wake. Na kwa mara ya kwanza nchini Tanzania tuliona Rais aliye madarakani akishinda kwa asilimia isiyozidi 70. Yote hayo ni ya kweli. Lakini pia tumeona kitu kingine cha tofauti – hali ya siasa baada ya uchaguzi!

Katika miaka mingine yote tulizoea kuona vyama vya upinzani “vikipotea” mara tu baada ya uchaguzi. Hali hii ilikifanya chama kinachokuwa madarakani na serikali yake vikifanya kazi kwa “ku-relax” – kwa raha zake. Vyama vya upinzani vilikuwa vikitoweka katika ulingo wa siasa na kuibuka tena miaka minne baadae. Hii iliwafanya hata wale waliokuwa madarakani kufikia hatua ya kuviita vyama vingine eti “vya msimu” – seasonal political parties. Hali hii imebadilika kabisa na sasa walio madarakani hawajui wafanye nini kuikabili.

CHADEMA mara tu baada ya uchaguzi hawakulala. Walijipanga kimkakati kwenda nchi nzima wakiwaelimisha wananchi juu ya matatizo yao na umuhimu wa kuwawajibisha viongozi wao. CHADEMA wanapita huko na huko wakiwaambia wananchi mapungufu na madhaifu ya serikali yao. Lengo la CHADEMA, na kwa hakika lengo la chama chochote cha upinzani duniani, ni kutafuta udhaifu wa chama na serikali inayotawala na kutumia udhaifu huo kuingia madarakani. CHADEMA wakikakaa na kusubiri uchaguzi mwingine hawataweza kuifikisha elimu ya kisiasa kwa wananchi, wananchi hawatafunguka macho na utawala utaendelea kuwa wa CCM. Hilo halina ubishi na hilo ndiyo hofu kuu waliyonayo CCM na serikali yake.

Wanachotakiwa kufanya CCM/Serikali:

Ili kukabiliana na wimbi hili la mapinduzi/mabadiliko linalotembea nchi nzima kwa sasa, serikali haitakiwi kufanya makosa wanayofanya sasa hivi. Kosa la kwanza ambalo serikali inafanya ni KUFANYA SIASA (kama CHADEMA) kuliko KUFANYA MAENDELEO. Huu ni mwanzo wa kupoteza vibaya. Badala ya kuingia kwenye ulingo wa siasa, serikali inatakiwa ijikite kwenye shughuli za maendeleo zenye kuonekana. Fanya juhudi nzito ya KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA na uusambaze huo umeme kwa wananchi kwa bei nafuu. Zibane mamlaka za maji na uhakikishe wananchi wanakuwa na VYANZO VYA UHAKIKA VYA MAJI SAFI NA SALAMA – mjini na vijijini. Kaza program ya UJENZI WA MABARABARA (RELI) nchi nzima kwa kasi ya kutisha. Weka vizuri vitengo vya mipango-miji kwa kuanzisha MAKAZI BORA na kupunguza FOLENI katika barabara za mijini. Fukuza kutoka kwenye chama na ndani ya serikali WATENDAJI WAZEMBE NA WALA-RUSHWA. Acha Kiswahili cha “tuache tu mahakama na vyombo vyetu vya sheria viwashughulikie.” – lini? Kwa mkakati wa namna hii CHADEMA haitawanyima usingizi. Hamtatumia mabilioni ya shilingi kujinadi wakati wa kampeini. Hiyo ndiyo akili.

CHADEMA

Posted on

It is election year in Tanzania and you can easily tell the hotness of the political milieu here in the country. Last night the largest opposition party in the country, CHADEMA, picked their candidate for the forthcoming general elections. This blog would like to take this opportunity to congratulate CHADEMA for their choice of a candidate. Unlike other parties’ candidates, Dr Wilbroad Slaa (pictured) will indeed pose a hurdle to the ruling party, CCM. He is a good leader and we can’t wait to see how he handles his new challenge.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.