
Jina la kwenye vitabu la mti (pichani kushoto) ambao babu Ambilikile Mwaisapile anautumia kuwatibu watu wenye magonjwa sugu ni Carissa edulis. Miaka michache iliyopita taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu ya Kenya (KEMRI) iliwahi kuufanyia utafiti mti huu. Watafiti wa Kenya walichokiona baada ya utafiti ilikuwa ni uwezo mkubwa wa mizizi na magome ya mti huo kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu. Hongera Babu.