RSS Feed

Tag Archives: Afrika

Ya Nyerere na Franco (Lwambo): Ni ili tufurahi tu?

Posted on

franco

nyerere1

Jumatatu ya tarehe 12 October na Jumatano ya tarehe 14 October zilikuwa siku maalum na muhimu kwa wana wa Afrika. Ni siku ambazo bara zima hata nje ya bara wote wapenda Afrika tuliungana kukumbuka watu muhimu katika historia ya Afrika ambao hatunao tena.

Jumatatu alikuwa akikumbukwa gwiji la muziki barani Afrika Franco Luambo Luanzo Makiadi aliyefariki yapata miaka ishirini iliyopita. Na siku moja baadae akawa anakumbukwa kipenzi cha wengi, mwanasiasa mahiri, mpigania uhuru na mzalendo wa Afrika, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwa Nyerere ilikuwa kumbukumbu ya miaka kumi tangu atutoke.

Wengi tunamjua Nyerere na sifa kemkem alizojipatia kama kiongozi shupavu wa Tanzania na bara la Afrika. Wengi (ama si wengi sana) pia tunamfahamu marehemu Lwambo Lwanzo Makiadi “Franco”, gwiji wa muziki si tu wa Congo bali wa bara zima la Afrika.

Hawa wawili walikuwa ni watu wa aina tofauti kabisa — mmoja alikuwa mwanasiasa na mwingine alikuwa mwanamuziki. Ila wawili hawa walikuwa na jambo moja walilofanana – walikuwa wazalendo na wapenda Afrika wa kweli.

Katika uhai wake, Lwambo aliwahi kuulizwa na Wamarekani kama angependa kushirikiana nao katika mradi wa muziki wa dunia. Wazungu hawa walitaka kuwakusanya wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kuwaweka pamoja ili waimbe pamoja na iweze kupatikana album moja itakayoitwa “Muziki wa Dunia”. Lwambo Makiadi alikataa. Sababu yake ilikuwa hii: “Mimi ni Mwafrika, ninaimba nyimbo za Kiafrika na asili ya muziki ni Afrika; kwa hiyo kama mkitaka njoo mchukue mziki wangu mpige maana huo ndio muziki wa dunia.” Wazungu wale wakarudi kwao na idea yao.

Msimamo wa Nyerere juu ya ushirika uliokuwa ukijulikana kama Pan-Africanism (Uafrika ama uzalendo wa Kiafrika) ulikuwa dhahiri. Aliiona Afrika kama moja na Waafrika kama ndugu. Hakuamini hata siku moja kwamba maendeleo ya Afrika yanaweza kuletwa na Wazungu au Wachina au Waarabu. Aliamini kwamba maendeleo ya Afrika yataletwa na Waafrika wenyewe.

Wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya watu hawa muhimu kwa historia ya Afrika kuna wengine wetu waliozichukulia, na wanaoendelea kuzichukulia hata sasa, kazi za magwiji hawa kama burudani tu. Wanasikiliza hotuba za Nyerere wanacheka tu, wanaburudika, wanafurahi. Basi. Hawaendi zaidi ya hapo. Wanapiga nyimbo za Lwambo, wanacheza, wanacheka, wanafurahi basi.

Hapana. Nyerere na Luambo (Lwambo) hawakuwa waburudishaji tu.

Viongozi wa Kiafrika na vipaumbele (Leadership and Priorities in Africa)

Sustainable energy is still a huge problem across Tanzania

Sustainable energy is still a huge problem across Tanzania

Nakumbuka mtangazaji mmoja maarufu wa VOA aliwahi kuja Afrika kufanya interviews na marais wetu. Mojawapo ya maswali aliyokuwa akiuliza lilikuwa hivi: “Mheshimiwa Rais, umekuwa kiongozi wa nchi hii kwa kipindi kirefu sasa; ni jambo gani moja tu ambalo unadhani wananchi wako watakukumbuka kwalo?

Kitu ambacho kilimshangaza sana yule mtangazaji ni kwamba karibu marais wote wa Afrika aliowahoji (wakiwemo wastaafu), hakuna aliyeweza kujibu swali hilo kiufasaha.

Marais wetu hawajui jambo moja (moja tu) ambalo wananchi wao watalikumbuka watakapokuwa wametoka madarakani. Hata wakishastaafu hawajui ni kitu kitu gani kimoja waliwafanyia wananchi na bado kinakumbukwa.

Kila aliyemwuliza alianza “Oh unajua nimefanya mambo mengi, siwezi kuyataja yote.” Na blah blah kibao.

Lakini tuseme tu ukweli. Marais wetu wanaingiaga madarakani bila malengo. Hakuna jambo moja ambalo anakuwa nalo kwamba angetaka kulifanya. Na madhara yake wanagusa kila kitu na mwisho wa siku wanakuwa hawajafanya lolote la maana.

Au wakiamua kufanya kitu, wanaibuka na madudu ambayo huwezi kupima mafanikio yake, kwa mfano MKUKUTA, MKURABITA, KASI MPYA, KILIMO KWANZA. Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuketi chini baadae na kupima kama vimefanikiwa au la – they are vague goals.

Ni tofauti na Rais ambaye anasema (tena kutoka moyoni) kwamba: “Mimi wakinichagua tu, nitahakikisha tunatandaza barabara za lami hadi kila makao makuu ya wilaya. Ndani ya miaka yangu kumi ya uongozi hata kama nitashindwa kila kitu ila nitahakikisha wilaya zote za Tanzania zinafikika kwa lami.” Sasa, huyo ni kiongozi.

Au mwingine anaweza akasema, “Mimi wakinichagua nitahakikisha kukosa nishati endelevu (umeme, gesi, solar, nk) hapa nchini kwetu inakuwa ni historia. Nitahakikisha tunapata umeme kwa gharama nafuu na nishati nyinginezo endelevu zinakuwa affordable.”

Wito na ombi langu ni kwamba ifike wakati sisi tunaokimbilia kugombea nyadhifa mbalimbali tujiulize: hivi ni nini nitalifanyia taifa langu endapo nitachaguliwa? Nitafanya jambo gani moja ambalo nitakumbukwa kwalo?

Ni jambo moja tu. Sio mambo lukuki.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.