RSS Feed

WATANZANIA: Tumejidanganya na sasa tunalia

Posted on

(almost) Kila mtu  analalamika. (almost)Kila mtu  ananyoosha kidole kwa mwingine. Hakuna anayetaka kubeba lawama. Hata tunapokosa wa kumlaumu tunailaumu serikali. Ili mradi kila kisichoenda kisichoenda kina wa kumsingizia kwacho. Kama unabisha soma magazeti ya leo: “Makosa ya Ngeleja”, “makosa ya Malima”, “makosa ya wizara”, “makosa ya serikali”, “makosa ya JK” au “makosa ni ya Jairo.” Hivi ni kweli? Si kwamba makosa ni yetu wananchi?

 

OK. Ngoja niseme hivi: ni nani amewafanya watu wetu kuamini kwamba PESA ni kila kitu? Ni nani amewafanya Watanzania kuamini kwamba ukiwa na gari na nyumba nzuri basi wewe umefanikiwa — umeukata? Ni nani? Ni nani aliyewaaminisha Watanzania kwamba ubora wa maisha umo katika wingi wa vitu mtu anavyomiliki? Ni nani?

 

Hakuna Mtanzania anayewaza ku-pursue dream siku hizi. Kila mtu anawaza atakavyopata pesa. Ni ugonjwa mbaya na tusipoangalia utatumaliza. Vijana wanapoajiriwa wanawaza jinsi ya kutoka — wanatafuta vimbinu vya kiwiziwizi ili mradi tu na wao watoke. Na tunapowaona wametoka hata hatajiulizi kwamba wametoka vipi. Tunawapigia saluti. Tunawaabudu na kuwasujudia. Hata kama ni wadogo, tunawaita “wazee”. Kisa? Wametoka. Wametokaje? Hatutaki kujua. Ila ni kweli kwamba hatujui?

 

Siku hizi hakuna Mtanzania nayetaka kuongelea integrity (uadilifu). Na ukitaja tu mambo ya uadilifu uaonekana wa zamani kwelikweli — unachekwa. Unaonekana kama vile umeshuka kutoka Mars! Watu wanatafuta vipato vya kipuuzi kwa nguvu zote — hata kama ni kwa kudanganya. Tumekuwa taifa la waongo, matapeli, wadanganyifu, wasingiziaji, walalamishi, wasiopenda kufanya kazi. Tunaingia ofisini, tunasaini halafu tunatoka kwenda “lunch”. Tukiulizwa tunacho kisingizio: UMEME. Wewe ni mfagiaji wa baraza umeme unahusika nini na kazi yako?

 

Siku hizi hakuna Mtanzania anayeongelea EXCELLENCE (ufanisi). Tunafanya vitu feki, tunauza vitu feki, tunaishi maisha feki, tuna mahusiano feki — tunaishi UONGO na NJIA ZA MKATO! Tunataka kutajirika haraka. Hatutaki kuumia. Tunataka kujenga maghorofa kwa njia za mkato. Hata madaktari hospitalini wanawatibu wagonjwa wao kwa njia za mkato — ili mradi pesa imeingia. Hakuna anayejali. Hakuna anayefanya kazi ili a-excel hapo kazini kwake. Watu wameridhika na MEDIOCRITY (kawaida). Tuna walimu wa kawaida, maprofesa wa kawaida, mainjinia wa kawaida, wanasheria wa kawaida, madaktari wa kawaida, fundi makenika wa kawaida, wakurugenzi wa kawaida, mawaziri wa kawaida. Hakuna unayemwangalia na kusema: excellent!

 

Matokeo yake ndo haya: tunaishi gizani, hatuna maji ya bomba, barabara nzuri ni za kuhesabu, watoto wetu wanakaa chini wanapokuwa shuleni, foleni, nk. Wa kulaumu ni sisi wenyewe. Tumewaabudu matajiri, tumeiabudu pesa na tunalia.

About Mwemezi

I am Tanzanian. I live and work in Tanzania. I work as a researcher in Environment, Sustainability and Development. I speak Swahili and a little bit of English ;) Welcome and have fun.

2 Responses »

  1. Tito Simon Tinuga

    Hizi nazo ni kati ya pumba maana unataka mtanzania aliyezaliwa leo ahukumiwe kwa dhambi ambayo hajaitenda. What am saying here…huwezi kumlaumu mtu wa miaka hata 30 kwa makosa yanayofanywa na watu wenye miaka 60 na 70 huko serikalini. huyu wa miaka 20 ajilaumu kwa lipi. There is no point in saying “Watanzania”….this article umeweka tu ili na wewe uwe kwenye wbsite ila haina thoughtful mind behind it! Pure madness and nonsense!

    Reply
  2. mzalendo wa kweli

    jitahidi hata kuangalia vichekesho vya comedy kipengele cha PIGA CHINI KINGEKUSAIDA kujua kwa nini wabadhirifu wanastahiri kupigwa chini. Hebu ona MLALAHOI anamudu kuchimba kisima cha maji chumvi anauza Tsh 50 serikali yenye dhamana,tuipayo kodi zetu inaposhindwa tuisifu au tuilaumu
    ishu sio chama ishu ni kuwakumbatia wanaoboronga, tunowakabidhi miradi hai mwisho wa siku wanatukabidhi magofu,madeni, na mabaki mengineyo

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.