RSS Feed

Kama ningekuwa Kiongozi wa “Chama”/Serikali

Posted on

Hivi karibuni nchi yetu imeshuhudia sarakasi za kisiasa zinazozihusisha pande mbili. Upande mmoja ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) au serikali na kwa upande mwingine ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa yule (yeyote) ambaye amekuwa mfuatiliaji wa siasa za Tanzania tangu ulipoingia mfumo wa siasa za vyama vingi hapa nchini atakubaliana na mimi kwamba kwa sasa mazingira ya kisiasa ya nchi yetu yamebadilika sana. Mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 tulishuhudia chaguzi ambazo zilivihusisha vyama vingi. Ukilinganisha na chaguzi zote za nyuma, ule wa 2010 umekuwa ni uchaguzi ulioibua mambo mengi.

Kuna watu ambao hawakuridhishwa kabisa na namna ambavyo Tume ya Uchaguzi ya Tanzania ilisimamia uchaguzi huo. Kuna ambao wanasema hadi leo kwamba asilimia ya wananchi iliyojitokeza na hatimaye kumchagua Rais ilikuwa ndogo kiasi ambacho kinatia doa (mashaka) ushindi wake. Na kwa mara ya kwanza nchini Tanzania tuliona Rais aliye madarakani akishinda kwa asilimia isiyozidi 70. Yote hayo ni ya kweli. Lakini pia tumeona kitu kingine cha tofauti – hali ya siasa baada ya uchaguzi!

Katika miaka mingine yote tulizoea kuona vyama vya upinzani “vikipotea” mara tu baada ya uchaguzi. Hali hii ilikifanya chama kinachokuwa madarakani na serikali yake vikifanya kazi kwa “ku-relax” – kwa raha zake. Vyama vya upinzani vilikuwa vikitoweka katika ulingo wa siasa na kuibuka tena miaka minne baadae. Hii iliwafanya hata wale waliokuwa madarakani kufikia hatua ya kuviita vyama vingine eti “vya msimu” – seasonal political parties. Hali hii imebadilika kabisa na sasa walio madarakani hawajui wafanye nini kuikabili.

CHADEMA mara tu baada ya uchaguzi hawakulala. Walijipanga kimkakati kwenda nchi nzima wakiwaelimisha wananchi juu ya matatizo yao na umuhimu wa kuwawajibisha viongozi wao. CHADEMA wanapita huko na huko wakiwaambia wananchi mapungufu na madhaifu ya serikali yao. Lengo la CHADEMA, na kwa hakika lengo la chama chochote cha upinzani duniani, ni kutafuta udhaifu wa chama na serikali inayotawala na kutumia udhaifu huo kuingia madarakani. CHADEMA wakikakaa na kusubiri uchaguzi mwingine hawataweza kuifikisha elimu ya kisiasa kwa wananchi, wananchi hawatafunguka macho na utawala utaendelea kuwa wa CCM. Hilo halina ubishi na hilo ndiyo hofu kuu waliyonayo CCM na serikali yake.

Wanachotakiwa kufanya CCM/Serikali:

Ili kukabiliana na wimbi hili la mapinduzi/mabadiliko linalotembea nchi nzima kwa sasa, serikali haitakiwi kufanya makosa wanayofanya sasa hivi. Kosa la kwanza ambalo serikali inafanya ni KUFANYA SIASA (kama CHADEMA) kuliko KUFANYA MAENDELEO. Huu ni mwanzo wa kupoteza vibaya. Badala ya kuingia kwenye ulingo wa siasa, serikali inatakiwa ijikite kwenye shughuli za maendeleo zenye kuonekana. Fanya juhudi nzito ya KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA na uusambaze huo umeme kwa wananchi kwa bei nafuu. Zibane mamlaka za maji na uhakikishe wananchi wanakuwa na VYANZO VYA UHAKIKA VYA MAJI SAFI NA SALAMA – mjini na vijijini. Kaza program ya UJENZI WA MABARABARA (RELI) nchi nzima kwa kasi ya kutisha. Weka vizuri vitengo vya mipango-miji kwa kuanzisha MAKAZI BORA na kupunguza FOLENI katika barabara za mijini. Fukuza kutoka kwenye chama na ndani ya serikali WATENDAJI WAZEMBE NA WALA-RUSHWA. Acha Kiswahili cha “tuache tu mahakama na vyombo vyetu vya sheria viwashughulikie.” – lini? Kwa mkakati wa namna hii CHADEMA haitawanyima usingizi. Hamtatumia mabilioni ya shilingi kujinadi wakati wa kampeini. Hiyo ndiyo akili.

About Mwemezi

I am Tanzanian. I live and work in Tanzania. I work as a researcher in Environment, Sustainability and Development. I speak Swahili and a little bit of English ;) Welcome and have fun.

6 Responses »

  1. Niukweli usiopingika kuwa usipoziba ufa utajenga ukuta ni hali halisi na changa moto kwa serikali iliyoko madarakani kutumia muda mwingi kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii nchi iko katika giza,malipo ya dowans,huduma mbovu za usafiri wa reli ya kati,mlipuko wa mabomu Gongo la MBOTO.HIZI ni changa moto zinaziotakiwa kutatuliwa na viongozi na si vinginevyo.

    Reply
  2. MBIU YA MYONGE.Kila mwanadamu ana matatizo yake binafsi.Kijana mmoja alikuwa akilala mika kwanini ameshindwa kunununa viatu ili afanane na wenzake shuleni, kisha kamweleza jirani yake ambaye yeye mwenyewe hajawahi kuvaa viatu tangu azaliwe,”tatizo si kununua viatu sina miguu hivo viatu nita vivaa wapi hivo viatu? Yule kijana kugundua hilo katulia kimya kwani matizo ya mwenzake ni zaidi ya yale yanayomsibu yeye.

    Reply
  3. nashindwa kuelewa dhamira ya wabunge wa ccm utakuta mbunge wa upinzani bungeni akikosoa wizara flani kwa maendeleo ya taifa watatafuta kila namna wapinge pia wapige makofi kwa wingi linanitatiza sana kujua dhamira yao kwa taifa big up sana waziri membe kwa bunge la jana

    Reply
    • Yes, Idd
      Wabunge wa CCM wao wapo kupinga kila hoja itakayotolewa na upande wa upinzani. Hata kama hoja hiyo ina maslahi kwa taifa. Cha kusikitisha ni kwamba baadae wanakuja kukuta ile hoja ilikuwa ya muhimu hivyo wanaiweka kwenye ilani yao ya uchaguzi unaofuata.

      Reply
  4. Mgomo wa madaktari Tanzania, Leo nazungumzia suala la mgomo wa madaktari hapa kwetu Tanzania nchi yenye raslimali nyingi lakini wanao faidika ni wachache. Posho ya siku moja kwa daktari mmoja shilingi 10,000 /= huyu ni mtu muhimu sana kwani huokoa maisha ya watanzania walio wengi ambao wangeweza poteza uhai . Serikali hutumia fedha nyingi kununua magari ya kifahari na kulipa posho waheshimiwa wabunge kiasi cha shilingi laki mbili kwa siku . Chondechonde jamani wananchi wanayaona haya maovu yanayotendwa hususani pale inapotokea kero ya ongezeko la gharama za umeme hii huathiri maisha ya watu wenye kipato cha chini hivyo basi umasikini wa watanzania utaisha lini iwapo hali itaendelea udumaza uchumi wa nchi. Lazima ifike wakati ambao kila mtanzania ataamua kuchukua hatua na si vinginevyo ni maandamano ambayo hupingwa na viongozi walioko madarakani.

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.