
Hmmmm; ugali samaki na vimaharage kwa pembeni. Hapo je?
Acha nikuulize swali la kizushi: Mara ya mwisho kula ugali ilikuwa lini? Hahaha. Kama upo hapa nyumbani litakuwa ni swali rahisi kwako ila kama upo ughaibuni, linaweza kuwa swali gumu sana kwako.


Ebwana hapo umenikumbusha nyumbani kabisa,maana huo msosi si wa kitoto yani hapa udenda unataka kutoka maana huku ughaibuni kidogo inakuwa ni ngumu,ila jamani ugali na umma ile kibongo sijaona mie.
Ally,
Chakula cha Kibongo kina mambo yake kaka. Na hapo unaona umma na kisu kwa sababu tu nilienda kwenye hoteli fulani fulani hivi. Ila ukinikuta home, ninakamata tu kwa mkono. Hahaha
chukua msosi wa kinyaru huo