Mapinduzi ya daladala

23 11 2009

Leo wakati nakuja katikati ya jiji la Dar es salaam nilipata bahati ya kupanda ‘daladala’ nzuri yenye heshima na utulivu. Huwa ninatokea kituo ama cha Davis Corner (Tandika) au Mwembeyanga. Nyakati za asubuhi katika vituo nilivyovitaja hapo juu hali ya usafiri kwa kweli huwa ni mbaya sana. Si rahisi kupanda gari kwa ustaarabu bila kusukumana na hata wakati mwingine kuibiwa vitu vyako.

Nilipofika Mwembeyanga leo nikamkuta kijana kama kawaida akipiga debe, “Posta, posta moja kwa moja mia tano. Posta mia tano moja kwa moja hiyoooooo.” Ilikuwa ni gari aina ya Toyota Coaster nzuri imesafishwa na viti vizuri vya kukalia. Kwa kweli ilikuwa inavutia. Sikuona kwa nini nisilipe mia tano na kutumia usafiri wenye ustaarabu kuliko kung’ang’ania kulipa 250 na kukipata cha mtema kuni.

Nilichokuja kugundua baadae ni kwamba huyu bwana alituleta mjini leo si yeye peke yake anayefanya hivyo. Wako wengi. Ila cha kusikitisha ni kwamba wanafanya kazi hii kwa kujificha. Swali ninalojiuliza ni hili: Kwa nini wasitangaziwe kwamba kama kuna mtu ana gari lake zuri nyakati za asubuhi wakati kuna shida ya usafiri ni ruhusa kupeleka watu mjini kwa gharama yoyote ambayo abiria wanaosubiri watakuwa tayari kulipa? Ningekuwa mhusika wa mambo ya usafiri katika jiji la Dar es salaam ningetoa tangazo la hivi:

“KAMA UNA GARI YAKO NZURI NA UNGEPENDA KUPAKIA ABIRIA WAKATI KUNA SHIDA YA USAFIRI (HASA ASUBUHI NA JIONI) UNARUHUSIWA KUTANGAZA KIASI CHOCHOTE CHA NAULI AMBACHO ABIRIA WATAKUWA RADHI KULIPA ILI UWAPELEKE WAENDAKO”.

Kwa namna hii tutasababisha ushindani wa wenye magari kuwakimbilia abiria wakiwaomba wapande magari yao na hii adha ya abiria kugombea magari itaisha. Pia hata wenye magari yao binafsi ambao huwa wakitoka kazini anaingia yeye mwenyewe na kuendesha gari la watu sita akiwa peke yake wanaweza kuwa wakitafuta walau mchango wa mafuta kwa kupakia abiria wawili au watatu nyakati za asubuhi au jioni.

KILIMO KWANZA!





Kutoka porini

21 11 2009

Enzi hizo tukijifunza kutumia digital -- 2005 Serengeti Nationala Park





‘Ikulu’ yetu

21 11 2009

<span style="font-family:comic sans ms;font-size:x-large;">Makazi Mapya</span>





Kombe ili tupige nalo picha?

21 11 2009

Hivi karibuni tumeshuhudia kombe la dunia likiletwa hapa kwetu ili Watanzania tupate “nafasi ya kuliona na kupiga nalo picha” Huu si ulimbukeni? Sasa tukisha piga nalo picha ndo inakuwaje? Pelekeni ujinga wenu huko. Kama hatuwezi kucheza soka tunadhani kwa kuliona kombe la dunia na kupiga nalo picha tutapata raha?

Kuona tu?





Ushauri wa bure kwa Ngeleja

21 11 2009

Kwa wale mnaofuatilia mambo ya Tanzania kwa karibu mtakumbuka kwamba hivi karibuni taifa lilikumbwa na mgao wa umeme. Japo ni vigumu kusema kama mgao huu umeisha ua la ila hali kwa sasa hivi (hasa hapa katika jiji la Dar es salaam) hali kidogo ime-stabilize.

Katika mazingira ya Kiafrika na hasa ya Kitanzania mambo mengi hufanywa kwa mtindo wa zimamoto. Miali ya moto ikishazimwa huwa hatuhangaiki hata kidogo kwenda kuchunguza chanzo cha moto ili kuzuia majanga mengine kama hayo kutokea siku za usoni. Tunakaa halafu tunakuja kukutana na tatizo kama lile lile na tunalitatua kwa style ile ile kana kwamba hatujifunzi kutokana na matatizo.

Wakati hali ya umeme nchini ikiendelea kutengemaa, ingawa ni kwa muda tu, ningependa kutoa ushauri wangu wa bure kwa wahusika. Ninafanya hivyo nikijua kabisa kwamba blog hii inasomwa na viongozi na watu wengi walio katika nafasi za maamuzi serikalini (kwa taarifa nilizo nazo). Kwa Mh. Ngeleja ningependa kutoa ushauri kwamba hiki si kipindi cha kupumzika. Wakati hali ikiwa inaonyesha dalili nzuri ni wakati wa kuchakarika na kutafuta nini hasa chanzo cha kukatikatika kwa umeme hapa nchini na ukae na wataalamu wako mtengeneze mpango-mkakati wa kutatua tatizo hili mara moja na ya mwisho.

Huko mbele tunakoelekea wataalamu wa mazingira wanasema wazi kwamba hali ya hewa hasa kwa bara la Afrika haitakuwa nzuri. Maeneo mengi yatakumbwa na ukame usio wa kawaida. Mvua hazitakuwa za kutegemewa tena. Hiyo lazima itufanye sisi tulio katika sekta ya nishati kuwaza mara mbili — lazima tuwe na vyanzo vingine vya umeme ambavyo siyo vile vinavyotegemea maji (Hydro-power). Lazima tuje na njia mbadala na endelevu za kutatua tatizo hili. Tunaweza hata tukaanza kutengeza vinu vya umeme karibu na maeneo ambako makaa ya mawe yanapatikana. Tuanze pia kuwaza kuhusu madini yetu ya Uranium tuliyo nayo kama tunaweza kuyarutubisha na kuzalisha umeme kutokana na nguvu ya kiatomia (atomic). Tutafute (kwa dhati) wataalamu katika eneo la kuzalisha umeme utokanao na gesi. Kuna maeneo ya Songosongo kule nasikia kuna kiasi fulani cha gesi ambacho kinaweza kuzalisha umeme.

Pamoja na njia hizo hapo juu lakini pia tusisahau kuwa na mitambo mizuri ya dharura ya kuzalisha umeme ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme kuliko uwezo wetu tulio nao wa kuzalisha umeme kwa sasa.

Kwa sasa tuna uwezo (endapo vyanzo vyote vitafanya kazi katika kama inavyotakiwa) wa kuzalisha megawatt zipatazo 660. Tukiweza kununua mtambo mkubwa wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha megawatt, say, 800 kwa wakati mmoja na tukahakikisha huu mtambo uko katika hali nzuri na standby tutasahau kabisa tatizo la umeme.

Kwa ufupi ni kwamba tunatakiwa kujifunza kutokana na historia na tusiwe watu wa kurudia historia. Naamini hili liko ndani ya uwezo wa serikali yetu tukufu. Tanzania isiyo na tatizo la umeme inawezekana.

KILIMO KWANZA!





Fight Climate Change with Condoms?

19 11 2009

HAWA JAMAA WANAPENDEKEZA KWAMBA WATU WAGAWIWE KONDOM NA WAELIMISHWE JUU YA UZAZI WA MPANGO ILI KUINUSURU DUNIA KUTOKANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA. BONYEZA HAPA ILI UIPATE MWENYEWE.





Namwachia Mungu: Maana yake nini?

19 11 2009

Mara nyingi hapa bongo utasikia watu wakisema: “Ah, mi namwachia Mungu.” Lakini huwa sielewi huo usemi huwa una maana gani. Watu husema hivyo hasa pale ambapo huwa ama wamehisi au wanajua kwamba wamesingiziwa katika jambo fulani. Sasa kama umesingiziwa unamwachia Mungu ili iweje? Kwani Yeye Mungu ndo amesingiziwa au ni wewe? Why can’t you face the reality instead of playing a religious card? Na mara nyingi huwa nina wasiwasi kama wale wanaosemaga wamemwachia Mungu huwa ni kweli wamemwachia Mungu au wanasema tu ili tusiendelee kuwahoji. Natamani kujua maana ya kumwachia Mungu. Wewe unalisababishia taifa hasara halafu ukihojiwa unajifanya ‘religious’ ati unasema, “Mimi namwachia Mungu.” Mkome kabisa.





Chipusi kuku, makachumbari na mazagazaga mengineyo

18 11 2009

Machipusi kuku na firigisi zake





Maficho ya wadau siku za weekendi: Asante Jeff

18 11 2009

Hapa ni Tanzania jamani





Tangazo la mtaalam wa Mchwa

18 11 2009

Wataalam





Changamoto Zetu Afrika

17 11 2009

Kuna wakati huwa najiuliza kama kweli kuna haja ya kuwa na vyuo vikuu (higher learning institutions) katika Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. Kitu ambacho hunifanya nikajiuliza hivi ni hii kuwa na taasisi kama hizi lakini bado hatujaweza kutatua matatizo yetu hata yale madogo madogo.

Nimekuwa nikifutilia kwa karibu tatizo ambalo tunalo hapa Tanzania – la umeme. Mimi nilidhani kwamba tatizo hili lilikuwa limesababishwa na kukosekana kwa mvua. Ila juzi nikaambiwa wala haikuwa kimo cha maji kwenye mabwawa bali mashine zenyewe zilikuwa mbovu.

Ili kutengeneza hizi mashine waliagizwa ‘wataalamu’ kutoka Ulaya. Nikajiuliza: Hivi Kitivo cha Engineering pale UDSM (I beg your pardon, naambiwa siku hizi sio kitivo tena bali ni University College of Engineering) wanafanya nini? Ina maana tangu tuanze kufunza wataalamu mainjinia nchi hii hatujaweza kabisa kupata mtu anayeweza kukarabati mtambo wa kuzalisha umeme? Na hizo digrii za Electrical Engineering mnazotoa kila mwaka huwa zina mchango gani kwa jamii yetu? Kuna haja kweli ya kuwa na ‘College of Engineering’?

Tatizo ni nini?

?????????????????????





RAMANI KWENYE BLOGU YAKO?

16 11 2009

KWA WALE AMBAO TUMO KWENYE LIBENEKE LA BLOGU, MNAWEZA KUIFURAHIA HII FEATURE. UKIWEKA KITU KINACHOITWA clustrmap KWENYE BLOG YAKO UNAWEZA KUJUA WASOMAJI WA BLOGU YAKO WAKO WAPI KATIKA USO WA DUNIA. KWA UFUPI UNAWEKEWA KARAMANI KADOGO KWENYE BLOGU YAKO AMBAKO UKIKACLICK KANAKUONYESHA LOCATIONS ZA WASOMAJI WA BLOGU YAKO. NI FEATURE AMBAYO BINAFSI NAIPENDA SANA. ILA INABIDI UWE MVUMILIVU KWANI HIYO RAMANI INAKUWA UPDATED KILA BAADA YA MASAA 24 TANGU ULIPOIBANDIKA KWENYE BLOG YAKO. UKIITAKA HII, SOMA ZAIDI JINSI YA KUIPATA KWA KUBINYA HAPA AU ANDIKA http://www.clustrmaps.com/ KWENYE ADDRESS BAR YA BROWSER YAKO.





Tanzania flat

15 11 2009
(c)Mwemezi 2009

Mtoko wa beach





Uswidi wakati wa spring

13 11 2009
(c) Mwemezi 2009

Hili ua nililipiga picha katika mji wa Lund, Sweden kwenye Botanic Garden (Botaniskagård i Lund) :) Wakati wa spring mwaka huu.





I LOVE TOKYO, lol

13 11 2009
belongs to Mwemezi

Eti: Ai lavu Tokyo. Daladala bwana!





KAZI KAZI KAZI

13 11 2009

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wametangaza kazi kibao kwenye website yao.

Au bofya hapa uzione





Germany’s goalkeeper Robert Enke committed suicide after ‘keeping depression secret for fear their adopted daughter would be taken away’ – mirror.co.uk

12 11 2009

It is a sad story with a huge sense of love in it.

 

Click here to read.





Maafa! Mvua kubwa zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo wilayani Same, Kilimanjaro zimesababisha vifo vya watu wapatao 20.

12 11 2009

Kwa habari zaidi bofya hapa





I love Tanzania

10 11 2009

ASANTE SANA MSOMAJI WANGU WA SERONERA (SERENGETI) KWA KUNITUMIA HII:

By Chunde, Serengeti 2006

Fahari yetu





Weekly countdown

10 11 2009

The following is a summary of people who hit this site from November 3rd to November 10th, 2009. I thank you for visiting my blog. I was especially touched to see a hit from Hong Kong, Pakistan and Poland. Thank you guys in the US — it’s an interesting turn-up — percentage-wise. For my fellow Tanzanians, I say Big Up sana tu.

Tanzania, United Republic of (TZ) 21
United States (US) 12
United Kingdom (GB) 4
Portugal (PT) 3
Sweden (SE) 2
France (FR) 1
Kenya (KE) 1
Denmark (DK) 1
Europe (EU) 1
Poland (PL) 1
Switzerland (CH) 1
Pakistan (PK) 1
Hong Kong (HK) 1
Japan (JP) 1
Australia (AU) 1
Italy (IT) 1
India (IN) 1




Hatuhitaji muujiza katika hili

10 11 2009

Ukipita mitaa ya Posta jijini Dar es salaam utashtushwa na majengo marefu yanavyozidi kujengwa katika maeneo haya. Sababu kubwa ya kuwa na foleni maeneo ya katikati ya mji ni asilimia kubwa ya watu kuingia katikati ya mji ili kufuata mahitaji yao mbalimbali. Kama watu wetu wanaohusika kutoa vibali vya kujenga wangekuwa na akili, katu wasingeruhusu kuendelea kujenga mighorofa hii katikati ya jiji. Wangetoa vibali vya ujenzi kwa wale wanaotaka kujenga nje ya Posta na Kariakoo.

Unapojenga maghorofa katikati ya jiji ni kwamba unafanya ofisi nyingi ziendelee kuendesha kazi zake katikati ya jiji na hivyo kusababisha misongamano isiyo ya lazima. Halafu hawa jamaa wakianza kujenga wanafunika zile site zao za ujenzi kwa ukuta wa mabati na kufanya barabara zetu ambazo tayari ni finyu kuzidi kuwa finyu. Acheni ujinga huu.





Nilikokuwa

9 11 2009
(c) Mwemezi

Salam nyingi toka Kijiji cha Kipepeo





Samahani wadau sijaonekana kama siku mbili tatu hivi. Nilijipa kalikizo kadogo. Unajua tena mambo ya mujini. Unakuwa biiiiize ila samtaimz inabidi ujipe mapumziko kwa afya. Nimerudi. Tuko pamoja.

9 11 2009




TP Mazembe 1-0 Heartland: Congolese Crows Clinch Third African Crown – Goal.com

7 11 2009

TP Mazembe may not be a name you know very well but it is a name which is known very well all over the D.R. Congo. A soccer team based in Lubumbashi City. Tonight they won the CAF trophy of 2009.

Click here to read more





Eastern DRCongolese: The Dancing Mourners

5 11 2009

I saw it when Mrs Clinton visited the area. But I didn’t give it a second thought. But then I saw it again when the UN boss responsible for refugees went to the area. People dancing. No, I mean Eastern D.R. Congolese dancing as a welcome gesture to their visitors. Then I started to think. I have seen (on TV) on several occasions when UN top officials or a US government top official made a visit to refugee camps in other parts of the world. There was a stark difference between how ‘our’ refugees welcome these officials and the way refugees in other parts of the world do it. In Asia and Eastern Europe you will see banners and protests remarking a visitation of the big shots. Refugees in these areas speak out their grievances outright — no sugarcoating. But refugees in camps in Africa will welcome their visitors with a dance and laughter. But when a reporter approaches the dancing refugees and ask them about their situation, the dancers start grieving — bitterly. And you wonder what was all the merriment for.

Image off Google

I WOULD MOURN, I WOULDN’T FAKE A LAUGHTER





Walking in the shoes of a star

4 11 2009

Recently in Tanzania, there has been a cluster of ‘talent search’ programs targeting youths all over the country. Copa-Coca Cola (football), Bongo Star Search (Music), Maisha Plus (Art), and Miss Tanzania (role model & beauty) to name but a few. While I am not against the act of searching for talents among Tanzania’s youths; I am however not happy about the aftermath of the projects. Although winners of these contests get lucrative prizes but one wonders how sustainable those prizes are especially considering that by participating in the contests, the standard of life of the contestant is ‘magically’ transformed to stardom. In some of these contests, it is actually the one who hits the jackpot (the winner) who receives something ‘tangible’. But if you look closely you realize that the level of fame of, say, the five finalists is more or less the same. What I usually ask myself after watching the finals of these contests is: “After we have made these guys very very very famous and gave only one them a prize, now what?” My point is: during the whole period of sieving the participants, these guys are exposed to ‘high life’. Come on, they are stars. So they live in five star hotels, they eat very luxurious meals, they shop in fancy malls and they have fans to clap hands for them while they perform. So after the project is finished, do we tell them, “thank you guys for coming and we wish you luck”? Do they go back to eating chai-maharage? I think it is time now we made a policy that sees that contestants (and especially finalists) in whatever talent search projects reap sustainable benefits in culmination. Organizers of these pageants and contests should be responsible in making sure that our stars remain to be stars even after the projects have ended.





Burekifasti ya Kibongo: Muhogo na chai ya maziwa

2 11 2009
(c) Mwemezi Rwiza

Karibu chai





Utalii wa Ndani na wadau wa Jo’Burg

2 11 2009
(c) Mwemezi 2009

Asante for making my day great on Saturday





Is there such a thing as a perfect ride on a daladala?

30 10 2009

You will never know where the next bump could be coming from when riding on daladala (City buses in Tanzania). This is definitely no place where you go to take a weight off your feet and enjoy the scenery as you are driven to your destination.

The other day I was lucky enougAnonymoush to be among the first people get into a small TOYOTA hiace going to Tegeta. I couldn’t beat window boarders, of course. By the time I got in there the back seat was already filled with men’s with smug looks on their faces.

I remember the Konda (bus conductor) warning them about not breaking his windows or they have to pay. So I was fortunate to get there way in advance and I had a two seconds window to choose a seat while the rest of the mob was still stuck at the door, all trying to get in at the same time.

There is no feeling like it really, that rush you get when you are among the first ones on board and there are seats spread out before you picking…………

Fighting the urge to thump my chest and roar in triumph, I quickly choose a place by the window and sat down. It was a double-seater and I calculated that the window spot would keep me safely away from the isle where I would have seen more likely to come into contact with the angry elbows and the tired bums of other passengers.

Plus I would have the freedom to open my window as wider as I wanted. Even with the spectre of swine flu there are people out there who would rather keep the window shut even on a crowded daladala. Makes you wonder about their priorities. I mean, a hairdo is expensive but swine flu…

I fished out my earphones and connected them to my phone. Now I was in my own world and for a moment it was possible to forget this was a daladala. Life was not bad at all!!

My thoughts were floating somewhere in paradise when suddenly WHAM! Something hit me on my face.

It was somebody’s plastic bag, the one which you are supposed to be fined with huge some of money if you are seen around with it. Fortunately this person was not carrying his hammer in that bag just some light stuff.

Still it was enough to knock my glasses half way off my face. I blinked several times and set my specks right.

Then I saw his face “sorre” he said.

I nodded. At least he was polite enough to apologise about it. What could you do when someone says they are sorry?

It was at that moment that the realisation hit me; there is NO such a thing as a glitch-free daladala ride. Wherever you sit or stand you are always vulnerable to some kind of knock. There I was celebrating my well-earned “perfect seat” on the bus and lost in beautiful music and something still had to happen as if to remind me I was on a daladala.

The person who had knocked my face was only reaching for somewhere to support himself as the bus began to move. He lost his balance and his hand instead landed on my head, the plastic bag knocked my specs.

Aside from the random smacks on the on the head from out of control arms, there are the strange protrusions on the body of the bus that are just waiting for the right opportunity to strike.

At first you will not even notice that there is a piece of metal jutting out just below the window. Then you will hear a familiar sound of something tearing (ohh your precious shirt) as you lean forward to hand over your fare.

Now you will have to shy away from the body of the bus with its cruel protrusions and sit right by the aisle… where the folding chairs are.

Unbeknownst to you, these little chairs can inflict a lot of damage when they are being folded to allow someone to pass.

When someone pulls up the chairs it will usually hit you in the elbow and anybody who knows elbows, knows how terribly they can hurt when knocked. This happens because after a certain point the chairs will snap into and the one pulling it will loose control of it. If your elbow is in the way then,  it will get a painful smack.

It all made me wonder whether perhaps we should all start to wear helmets with shin pads, knee pads and elbow pads as well before we get on the bus.

Article by:

epkalunga@yahoo.co.uk of The Guardian (Tanzania) *[Bracketed emphasis mine]*





Futuhi. Hawa jamaa mimi nawapenda kitu kimoja. Vichekesho vyao viko halisi mno. Halafu wanabadilika. Endeleeni hivyo hivyo Futuhi.

30 10 2009
Kwa hisani ya Star TV

Hongera kwa kazi nzuri





Hili la Ghana limenikuna

30 10 2009

JUZI MAWAZIRI NA VIZITO NCHINI GHANA WALIAMUA KUPAKI MAGARI YAO MAJUMBANI NA KUTUMIA USAFIRI WA UMMA (daladala) KWA AJILI YA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA. l
KWA MARA NYINGINE WAGHANA WAMETUONYESHA NI KWANINI WALIKUWA NCHI YA KWANZA YA AFRIKA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA KUTEMBELEWA NA RAIS MPYA WA MAREKANI. VIONGOZI WA BONGO; MMEIPATA HIYO?

SOMA ZAIDI KWA KIMOMBO HAPA:

Ghanaians, including Ministers of State and high profile personalities on Wednesday parked their cars and joined public transport to their various work places.

The Deputy Minister for Transportation, Dzifa Ativor said the campaign is to enable high profile public officials to experience the use of public transport and give the Ministry the chance to identify some of the problems of commercial drivers and the general public.

Madam Ativor who boarded a trotro to her office this morning told Radio Ghana her ride was not comfortable. The Minister of Roads and Highways, Joe Gidisu says the declaration of today as a Public Transport Day will enable public officials to feel what the ordinary man goes through in their daily activities.

Mr. Gidisu said government will implement an urban transport special project that will improve movement in the urban areas.

Meanwhile the General Manager of Metro Mass Transport, Martin Afram has expressed satisfaction with government for setting aside today as Public Transport Day as it coincides with Metro Mass Transport day.  He said the day will help the Metro Mass Transport to come out with solutions to some of the problems associated with public transport.

The campaign was to make public transports a reliable means of commuting to and from work.

The declaration of the day was announced at the launch of the tenth anniversary of the National Road Safety Commission at Gomoa Assin Mampong in the Central Region.

Posted on: Wednesday, 28, October, 2009
Source: GBC NEWS




Baadhi ya nchi za Kiafrika zilimwaga damu kujikomboa kutoka mikononi mwa wakoloni. Baadhi ya nchi zetu zitahitaji kumwaga damu kujitoa katika makucha ya mafisadi.

29 10 2009
Mwemezi

Utu wetu u wapi?





Tunamwitaji Dikteta

29 10 2009

Wachuuzi katika kituo cha mabasi cha Mwenge, Dar es salaam. Si wengi kati ya vijana hawa wanafanya kazi kwa tija.

Kama rasilimali tunazo. Watu tunao. Ardhi ya kutosha. Kwa nini mpaka leo hatuwezi kufanya hata mambo madogo kama kuwa na umeme wa kuaminika? Kwa nini bado watu wetu hawana maji? Kwa nini bado hatuna barabara? Kwa nini? Kwa nini bado sisi ni ombaomba? Kwa nini  bado viongozi wetu wakienda kwenye vikao wanaonekana ni wanyonge na waliokuja tu kutembeza bakuli la kuomba misaada?

Mimi nafikiri imefika Afrika tuchague viongozi watakaozifungia masikio kelele za nje na kuhakikisha Afrika inapiga hatua za kimaendeleo. Viongozi ambao watathubutu kufanya ‘what is right for their people’ hata kama World Bank itasitisha msaada. Viongozi watakaofunga migodi mpaka mwekezaji akubali kuchakata (to process) madini yote hapa hapa ndani ya nchi na kuajiri asilimia sabini (70%) ya wazawa kwenye nafasi andamizi za kampuni. Tunahitaji viongozi watakaosema kipaumbele cha serikali zetu ni kuona watu wametoka kwenye umaskini na si takwimu zisizo na mbele wala nyuma. Kiongozi atakayewalazimisha wananchi wake kufanya kazi na sio kuzunguka siku nzima na pea mbili za viatu mikononi kwa kisingizio cha ujariamali.

Kiongozi atakayeamka asubuhi na kusema: “Yesterday I couldn’t sleep, I had this terrible nightmare. I think my government is overspending. As of day one of the next month, we will sell all the luxurious cars we officials are using and instead we are going to buy cheap cars. The money raised from that sale will buy tractors and hire agricultural extension officers. I therefore ask my Minister for Finance to act accordingly. A team of financial experts need to go through all ministries and departments to make sure this is done in the most effective and incorrupt way. Thank you”.

All we need is a patriotic dictator.





Ningekuwa waziri ningechukiwa

29 10 2009

Kwanza nisingekubali matendo yaliyo kinyume na sheria na kanuni kufanyika hata kama hao wanaoyafanya ni ndugu zangu:

  • Ningekuwa waziri mwenye dhamana ya Usafiri au Usafirishaji ningehakikisha hivi vigari vyote vinavyoitwa vidaladala nimeviondoa mjini na badala yake nikatafuta watu wachache wenye akili wakabuni njia mbadala, iliyo na heshima, ya usafiri mijini.
  • Ningekuwa waziri anayehusika na Makazi au Mipango Miji ningehakikisha wote wanaoendesha biashara, ziwe halali au la, katika maeneo ambayo hayaruhusiwi wanaondolewa kwa nguvu na, kwa kushirikiana na majeshi yote ya nchi (polisi, mgambo, JWTZ, magereza) ningehakikisha kichapo wanachokipata kitawafanya wasithubutu kurejea kwenye maeneo hayo.
  • Ningekuwa waziri wa Ajira au Kazi ningeshirikiana na waziri wa Kilimo na kwa pamoja tungefanya program moja ambayo tungeiita “Nguvukazi”. Katika program hii vijana wote wanaolandalanda mijini bila lolote la maana wanalofanya ningewasomba kwenye makarandinga huku wamefungwa vitambaa vya macho na kuwapeleka kwenye ardhi yenye rutuba wakalime.
  • Ningekuwa waziri wa Mambo ya Ndani ningehakikisha kila Mtanzania ana kitambulisho kinachomtambulisha kwamba yeye ni raia wa Tanzania.

Ukifanya mambo kama hayo hapo juu si rahisi kupendwa ila wenye akili wataelewa ni nini unafanya.





Majengo marefu yanazidi kuongezeka Dar: Hii inaitwa Exim Tower. Iko pale mitaa ya Posta Mpya

27 10 2009
Copyright Mwemezi 2009

Anga linazidi kukwanguliwa tu





Lambalamba zinapita, mcheki huyu jamaa anavyokatiza kwenye foleni maeneo ya Morocco na kibaiskeli chake cha lambalamba

27 10 2009
picha mali ya Mwemezi

Si mchezo





Mtaani Kwetu

27 10 2009
(c) Mwemezi

Mtaani Kwetu





Dar Leo: Akiba shusha

27 10 2009
Akiba

Maeneo ya Akiba Dar es salaam





Karne ya 21 Jijini Dar

25 10 2009
Gari la kubebea maji ya kuuza -- biashara ya mtu

Gari la kubebea maji ya kuuza -- biashara ya mtu

Hii sasa inakupa picha huko vijiji upatikanaji wa hii huduma muhimu kwa maisha ya kila siku ukoje. Kama Dar kwenyewe tunategemea tankers za watu binafsi kutuuzia dumu kwa shilingi mia tatu. Je, uko Bukombe na Naliendele? Si balaa hii?





Lugha-Picha

25 10 2009
Hapa napo vipi?

Hapa napo vipi?





Magazeti ya Leo

25 10 2009
Magazeti ya Leo

Magazeti ya Leo





Mvua mvua mvua

24 10 2009
Mvua Mvua Mvu

Mvua Mvua Mvua





Mvua imeanza Dar

24 10 2009
Jiji la Dar es salaam leo limepata baraka za mvua

Jiji la Dar es salaam leo limepata baraka za mvua





Soccerlicious

23 10 2009
Timu ya Dunia. Big up, mates :)

Timu ya Dunia. Big up, mates :)

When leaders meet for the beautiful game





Siwezi kuacha kukupenda, Unapendeza Mwanza

23 10 2009
Mwanza jamani. I want to go back there. Rocky City

Mwanza jamani. I want to go back there. Rocky City





Cynthia: Our leaders do not read :)

22 10 2009

I was touched by the article in The Guardian (Tanzania) of October 19th, 2009 by Cynthia Stacey. She wrote about several things she observed while here in our ‘peaceful’ country — Tanzania. I will post her last few paragraphs which I found both amusing and educative.

“But before I close, what’s to do on my return … let’s see … Ah yes:

  • Suggest to good guy P.M. Pinda he reconstitutes the municipal councils, and sets up a working central alternative instead
  • Ask Tanroads boss Mr. Mrema what criteria were used to give only two companies exclusive rights to erect billboards, before we all suspect the reason
  • Find out how the new billboard and advertisement control regulation, 2009 (under the P.M.’s Office) will be properly administered, so what’s left of ravaged Dar es salaam, is people oriented, not billboard dominated
  • Request any of the four mayors to walk to the Post Office and see it they feel shame at the chaotic mess in front of, supposedly passenger bus stops, but taken over by phone card vendors etc. instead
  • Lobby gorgeous airport czar Prosper Tesha to pretty up J.N.I.A. (Julius Nyerere International Airport) to match the technical improvements in the offing.

Now this is the part I like the most about her article:

“As the first aspect of the country passengers see, the airport forms a definitive and lasting impression ironically, being very shabby and run down, it is currently an accurate barometer of the country, or many urban areas at least.

…. anyway, Prosper, me darlin, can you do a few cosmetic changes to your territory: a little paint, hanging plants, palms in pots, some good African art, but no more Kariakoo market style Chinese waste bins in departures please … we need a bit of class and sophistication , to equate with that descriptive word ‘international’ ….. bye”





Ah?

22 10 2009
Msimu wa tu-ku-tu-ku-tu-ku-tu-ku

Msimu wa tu-ku-tu-ku-tu-ku-tu-ku

Jana Mh. Rais ameagiza mitambo ya IPTL iwashwe ili kutunusuru na janga la giza totoro. Niliposikia hilo agizo lake nilishtuka kidogo. Kilichonishtua: 1) Ina maana ile mitambo ipo tu imezimwa wakati sisi tunalala gizani? 2) Mbona waziri wake juzi alidai kwamba amekuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa IPTL ili turuhusiwe kuibadilisha mitambo yao kutoka kutumia mafuta hadi kutumia gesi?

Mi nimechanganyikiwa.





Down the memory lane

21 10 2009
In Serengeti in 2005: L to R: Chunde, Anne, Mrs Chunde, Michael and Kiongozi

In Serengeti in 2005: L to R: Chunde, Anne, Mrs Chunde, Michael and Kiongozi

Ah. Siku zinakimbia sana. Hii ilikuwa mwaka 2005 wakati kiongozi anaishi Seronera, Serengeti.





Kiinglish: Kwani lazima?

21 10 2009
Filamu Zetu

Filamu Zetu

Hiki nacho ni kichefuchefu kingine. Sasa hivi wasanii wetu hasa wale waigizaji wa filamu pamoja na maprodyusa wao wameibuka na jipya. Filamu karibu zote wanazoigiza sasa hivi zinatoka kwa majina ya Kiingereza. Mwanzoni nilifikiri labda jamaa wanaongea kiinglish humo ndani. Kucheki nikakuta wanapiga Kiswahili muvi nzima. Sasa kwa nini wanaipa jina la kidhungu wakati kinachoongewa humo ni Kiswahili?

Majina ya filamu zinazotoka sasa hivi ni kama: Last Minutes, My Love, Don’t Hurt Me, n.k





Hongera Mr and Mrs Merahi Ahferom

20 10 2009

Blog ya viongozi inachukua nafasi hii kuwapongeza rafiki zetu wapendwa Merahi na mke wake mpendwa Zebib (wa Eritrea) kwa kufikisha mwaka mmoja wa ndoa yao. Harusi yao ilifanyika katika jiji la Lund, Sweden tarehe 19. October. 2008 na kiongozi alialikwa kama mtu wao wa karibu na mpiga picha wao mteule. Nawashukuru kwa upendeleo wenu. Mungu awabariki na awape maisha yenye furaha.

Merahi and Zebib. Congrats on your first anniversary

Merahi and Zebib. Congrats on your first anniversary